Saturday, September 10, 2011

Madhara ya punyeto kwa mwanaume


Ifahamike kuwa kuna watu wengi sana wanatumia mikono yao kujisaga katika sehemu nyeti, Jambo hili linamadhara makubwa sana kwa binaadamu, Jambo hili kwa lugha ya kiingereza wanaliita Masturbution, ni kitendo cha mwanaume kujisugua tupu zake.

Licha ya tafsiri ya punyeto kuwalenga wanaume zaidi lakini katika mada yangu ya pili nitaelezea Usagaji na madhara yake kwani hili linahusu wanawake na hili la usagaji linaingizwa na punyeto kwani madhara yake yanakaribiana lakini tofauti inakuja jinsi ya kujirizisha.

Wanaume wengi sana wanatumia mikono mikavu kujisaga, jambo hili huwafanya waharibu mishipa ya fahamu inayounganisha uume na mfumo uliopo kwenye ubongo.

Uharibifu huu humfanya mwanaume apoteze msisimko wa kujamiiana au hata akiupata humfanya ashidwe kufikisha hisia zake kisawasawa khasa akikutana na mwenza wake ambaye sehemu zake nyeti ni laini sana tofauti na mikono alozoea kujichua nayo.

Jambo jingine hatari linalo mkabili mpiga Punyeto ni upotevu wa hisia wakati wa kujichua kwa mfano ili afike kwenye kilele lazima akuze hisia zake kwa kiwango cha juu, pengine kupita ukweli halisi ataokutana nao pindi atakapokuwa na mwanamke faraghani.

Mpiga Punyeto hajitoshelezi mpaka amlete kwenye hisia mrembo kama Miss World kisha amvike utundu wa kimahaba ampe manjonjo hadi mwenyewe atosheke, kwa namna hii mwanaume mwenye kufanya mazoea ya kufanya hisia za wanawake warembo ambao hawezi kuwapata kwa hali halisi anapokutana na kina Mwafulani wa mtaani tena sio mtundu kimapenzi, hapo kamwe hawezi kusisimka mwili  na hivyo kujikuta Uume wake husimama kwa kiwango cha chini sana.

Madhara mengine yanayopatikana ndani ya kitendo hiki ni kuumwana sana na kichwa, mgongo, kupoteza nguvu za mwili na macho,  madhara mengine makubwa khasa mwanamme anaejichua mara mbili au tatu kwa siku  ni kushidwa kuzalisha, hii inatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume kwenye mfuko wa uzazi.

Hii yote madhara ya hapa duniani lakini kwa Allah ni mwisho wa hisabu kwani ''Amelaaniwa mtumiaji mkono kwa kujisugua uume wake(Punyeto)

No comments:

Post a Comment